1 Samuel 17:4-7

4 aShujaa aliyeitwa Goliathi, aliyetoka Gathi, akajitokeza kutoka kambi ya Wafilisti. Alikuwa na urefu dhiraa sita na shibiri moja.
Dhiraa sita na shibiri moja ni sawa na mita 3, au futi 9 na inchi 8.
5Alikuwa na chapeo ya shaba kichwani mwake, na alivaa dirii ya shaba kifuani mwake yenye uzito wa shekeli elfu tano.
Shekeli 15,000 ni sawa na kilo 50.
6 dMiguuni mwake alivaa mabamba ya shaba, na alikuwa na mkuki wa shaba mgongoni mwake. 7 eMpini wa huo mkuki ulikuwa kama mti wa mfumaji, na ncha ya chuma yake ilikuwa na uzito wa shekeli mia sita.
Shekeli 600 ni sawa na kilo 7.
Mbeba ngao wake alitangulia mbele yake.

Copyright information for SwhNEN